Song of Solomon 3:1-4

1 aUsiku kucha kwenye kitanda changu
nilimtafuta yule moyo wangu umpendaye;
nilimtafuta, lakini sikumpata.

2 Sasa nitaondoka na kuzunguka mjini,
katika barabara zake na viwanja;
nitamtafuta yule moyo wangu umpendaye.
Kwa hiyo nilimtafuta lakini sikumpata.

3 bWalinzi walinikuta
walipokuwa wakizunguka mji.
Nikawauliza, “Je, mmemwona
yule moyo wangu umpendaye?”

4 cKitambo kidogo tu baada ya kuwapita
nilimpata yule moyo wangu umpendaye.
Nilimshika na sikumwachia aende
mpaka nilipomleta katika nyumba ya mama yangu,
katika chumba cha yule aliyenichukua mimba.
Copyright information for SwhKC